logo

DAWASA TUPO TAYARI KUWAHUDUMIA WATEJA WETU WA VIWANDANI

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu Wa Maji Safi Na Usafi Wa Mazingira Dar Es Salaam (DAWASA) Bw.Kiula Kingu Ametoa Rai kwa maeneo yote ya viwanda jirani na eneo la mradi wa Maji Zegereni Uliopo Kibaha wanaohitaji huduma ya maji kwa ajili ya kuwekeza kwenye viwanda kuwa wapo tayari kuwahudumia.

.

Kingu Ameyasema Hayo Agosti 11,2023 Alipokuwa akizungumza Na Waandishi Wa Habari Kuhusu Utekelezaji Wa Majukumu ya Mamlaka hiyo Na Mwelekeo wake Kwa Mwaka Wa Fedha 2023/24 Katika Ukumbi Wa Idara Ya Habari Maelezo Jijini Dodoma.

.

Amesema DAWASA imejipanga kikamilifu na kuchukua hatua za makusudi za kuboresha usafi wa mazingira kupitia miradi mikubwa na midogo,Hii ni kwa sababu upatikanaji wa maji unapoongezeka unapaswa uambatane na usimamizi madhubuti wa usafi wa mazingira.

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu Huyo Amesema Mradi wa Chalinze awamu ya tatu uliojengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 94, umeweza kuongeza upatikanaji wa maji katika eneo la Chalinze kutoka asilimia 80 hadi 83 ambapo umeongeza upatikanaji wa huduma ya maji katika vijiji 87 zaidi.

.

"Mradi mwingine ni wa kujenga mfumo wa kukusanya majitaka na maeneo nufaika ambapo katika awamu hii ni Mbezi Beach, Kilongamwima, baadhi ya maeneo ya Kawe na Salasala. Utekelezaji wa mradi umeanza na Wakandarasi wanaendelea na shughuli za maandalizi ya ujenzi" Amesema Kingu.

.

Aidha,Kingu Amesema DAWASA pia imekuja na ubunifu wa kujenga mifumo na mitambo midogo midogo ya kuchakata majitaka inayojengwa maeneo ya pembezoni ambapo zaidi ya lita 780,000 za majitaka zitakuwa zikichakatwa kwa siku.

.

"Miradi hii itajumuisha ujenzi wa vyoo vya umma 30 ambavyo vitasaidia kuboresha usafi wa mazingira" Amesema.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn