logo

DKT.MPANGO: VIJANA WOTE JIEPUSHENI NA MATENDO MAOVU

Makamu wa Rais Mhe. Dkt.Philip Mpango Ametoa wito kwa Vijana wote nchini kujiepusha na matendo yoyote yasiyoendana na Maadili Yetu ya kitanzania.

.

"Matumizi ya Madawa ya Kulevya,Unyang'anyi,Mapenzi Ya Jinsia Moja,Rushwa,Utapeli, na Mengineyo" Amesema Mpango.

Mpango ameyasema Hayo Leo Agosti 07,2023 Jijini Dodoma Alipokuwa Akifungua Kongamano la Vijana linalofanyika Kuanzia Leo Agosti 7-8 Jijini Dodoma Katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Center.

.

Kwa Upande Mwingine, Mpango ametoa maagizo Kwa Ofisi ya Ortamisemi kuwaandikia Barua Wakuu wa Mikoa Yote Nchini ili waweze Kuandaa Makongamano ya Vijana katika Mikoa Yao Ili waweze Kujifunza mambo Mbalimbali na waweze kujikwamua Kiuchumi.

.

Makamu wa Rais amesema Taifa la Tanzania ni la Vijana, kwahiyo ni lazima Vijana walichukue taifa Lao kwa mikono miwili kwa kujituma kwa kufanya kazi.

.

"Hamlichukui taifa Lenu bila kufanya kazi, katika Sekta Binafsi au Ya Umma nendeni mkafanye kazi kwa Uadilifu na kwa kujituma, Bila kujibakiza.

.

"Sisi kazi yetu ni kuwaongoza ili kipindi chetu kinapokwisha tuhakikishe kwamba Mama Tanzania anabaki katika mikono salama. Nawaomba vijana kila mmoja akatimize wajibu wake" amesema Mpango.

.

Aidha, Mpango Ametoa Pongezi kwa Mkoa wa Dodoma kwa kubuni wazo Jema la kuandaa Kongamano la Vijana ambalo litasaidia vijana hao kujikwamua katika uchumi nk.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn