logo

CANADA YATOA SHILING BILIONI 93 SEKTA YA ELIMU TANZANIA

Serikali ya Nchini Canada imetangaza kutoa Kiasi Cha Shilingi Bilioni 93.14 za Kitanzania (Sawa na Dola za Canada milioni 50) kwa ajili ya kusaidia sekta ya elimu Tanzania.

Waziri wa Maendeleo ya kimataifa Bw.Harjit Sajjan ameyasema hayo leo Alhamis Julai 20, 2023 wakati alipofanya ziara katika Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Amesema kati ya fedha hizo Shilingi Bilioni 46.57 (sawa na Dola za Canada milioni 25) zitakwenda katika kuboresha upatikanaji wa fursa za elimu na ujuzi kwa mabinti wa Tanzania, kukuza uwezeshaji wake na kupata fursa za ajira za staha.

Sajjan amesema pia Shilingi Bilioni 46.57 (sawa na Dola za Canada milioni 25), zitakwenda katika mradi wa ‘Kila Binti Asome’ utakaotekelezwa na Shirika la Kimataifa la Watoto (UNICEF), Tanzania Bara na Zanzibar.

“Mradi huu utawezesha elimu kwa mabinti katika ngazi ya msingi na sekondari haswa katika masomo ya sayansi na hisabati,” amesema.

Naye Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda amesema kwa muda mrefu, nchi ya Canada imekuwa na ushirikiano mzuri na Tanzania.

“Tunafanya mageuzi makubwa ya elimu nchini. Wakimaliza shule ya msingi wakienda sekondari kutakuwa na mikondo miwili wa jumla na mikondo ya amali,”amesema Mkenda.

#JordanMediaUpdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn