WAZIRI AWESO AMTUMBUA MKANDARASI WA MRADI WA MAJI KAZURAMIMBA- KIGOMA
Waziri Wa Maji Mhe.Jumaa Aweso Amefanya maamuzi ya kumuondoa Mkandarasi wa Mradi wa Maji Kazuramimba Uliopo Mkoani Kigoma unaotekelezwa kwa Ufadhili waEnabel na Mkandarasi baada ya kutembezwa umbali mrefu bila kuona vituo vya Maji akiongozana na wananchi wenye hisia kali.
.
Aweso amefanya Maamuzi Hayo mara Baada ya kufika Kazuramimba Wilaya ya Kasulu-Kigoma katika mwendelezo wa Ziara yake ya kikazi, na hakufurahishwa wala kuridhishwa na kitendo cha Mradi wa Maji Kazuramimba kuchukua muda mrefu bila kukamilika wakati wananchi wakiendelea kuteseka na ukosefu wa huduma hii muhimu.
.
Aidha, Waziri Aweso Wakati wa ziara hiyo amekiri wazi kutoridhishwa na kasi ya Mkandarasi katika utekelezaji wa mradi huo ambao umeanza toka Novemba, 2020 na alitakiwa kukamilisha kazi katika kipindi cha miezi tisa na badala yake sasa ni mwaka wa tatu.
Kutokana na hali hiyo, Aweso ameivunja kamati ya Maji ya Mradi huo na kuitaka RUWASA kukamilisha mradi huo ndani ya kipindi cha siku 13 na kuusimamia.
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news