logo

KIWANDA CHA GESI SAFI KUJENGWA KIBAHA MKOANI PWANI

MKUU Wa Wilaya Ya Kibaha Mhe. Nickson Simon Leo April 20,2023 Amemwakilisha Mkuu Wa Mkoa Wa Pwani Mhe.Aboubakar Kunenge kwenye Uzinduzi wa Mpango wa kisasa wa Mkoa wa Pwani wa kusimamia mazingira ambapo Mgeni Rasmi akiwa Waziri wa Muungano na Mazingira Mhe.Selemani Jafo.

.

Katika Uzinduzi Huo, Simon Amesema Katika Mkoa Huo wamepanga kujenga kiwanda cha gesi safi Kibaha kwa kushirikiana na Taifa Gesi, Kiwanda cha Mkaa mbadala kwa kushirkiana na STAMICO, Wanafunga miundo mbinu ya Gesi (tayari wameshafunga mtungi wa Tani Moja Shule ya wasichana ya Ruvu) Na wamegawa mitungi ya Gesi kwa Akina Mamalishe Katika Mkoa Huo.

.

"Tunapanda miti milioni 15, tayari tumepanda miti milini tisa, tukishirikiana na TFS pamoja na NMB, Tuna tengeneza ajira mbadala wa biashara ya mkaa kwa vijana kupitia viwanda na Kilimo" Amesema Simon.

.

Aidha, Mkuu huyo Amesema Malengo ni kupunguza gharama za nishati kwa asilimia 40%, kuwaondoa wananchi katika matumizi ya mkaa na kuni, kutunza vyanzo vya maji, kujenga uchumi na jamii rafiki kwa mazingira.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn