WAZIRI UMMY AKABIDHI MAGARI 3 KWA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu (Mb) amekabidhi magari matatu ya Uokoaji ambayo yamenunuliwa na Wizara hiyo yenye thamani ya shillingi Bilioni 1.6 kwa Ajili Ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
Ummy amekabidhi magari hayo kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mhandisi Hamad Masauni (Mb) katika hafla iliyofanyika katika Viwanja vya Kituo Cha Zimamoto na Uokoaji Ilala (Fire) mapema Leo tarehe 8 Julai, 2023.
Aidha, Ummy amesema wao kama Wizara ya Afya wametoa magari hayo ili kupunguza vifo na majeruhi wengi wa ajali kutokana na kukosekana kwa vifaa vya uokoaji ikiwemo magari yenye vifaa maalum kama haya yaliyokabidhiwa hii leo.
Kwa Upande wake Mhandisi Masauni ameishukuru Wizara ya Afya kwa kuwapatia magari hayo ambayo yanaenda kuongeza tija na kuondoa changamoto zilizokuwa zikilikabili Jeshi hilo na kuahidi kuyatumia magari hayo ipasavyo ili kuhakikisha maisha na mali za watanzania vinakuwa salama.
"Tutahakikisha maeneo yote ambayo ni korofi kwa ajali za barabarani magari haya yatakuwa yanafanya patrol usiku na mchana" amesema Masauni.
@tanzimamoto
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

