MSANII MR.BLUE: B-DOZEN ANA MCHANGO MKUBWA SANA KWENYE SANAA YANGU
"B-Dozen Ni Mtu ambaye Ana Mchango Mkubwa Sana Kwenye Sanaa Yangu, Namshukuru Sana Kwenye Maisha Yangu, Nisipomtaja Nitakuwa Nakosea Sana.
.
Kipindi Nilipokuwa Kimya Katika Game, Natumia Mihadarati Nilipotea Kwenye Music So @bdozen Ndiye Mtu ambaye nilikuwa Najuana Nae Kitambo Tu na Tulikuwa Tunaendana Hivi, Alipoona Nimekuwa Kimya Katika Game Akawa ananiuliza Mbona Upo Kimya ...??. Nikamwambia Sielewi ila Nina Ngoma Naomba Nikupe wewe ukae Nayo ukiona inafaa utawapa Watangazaji, Ma-dj wengine waipige.
.
Baada ya Dozen Kumpatia Wimbo Wa #PESA Yeye Mwenyewe akasema "Hii Nyimbo Umekaa Nayo Ndani Tu Bila Kuiachia??", @blue Hii Ngoma Hapana Naomba Tuiachie Kabisaa.
.
Tanzania Nzima Single Ya #PESA Nilimpa @bdozen Peke Yake NaSikwenda Kwenye Interview Sehemu Yoyote Ile ila nilimkabidhi Yeye Tu Mpaka Ile Ngoma ikahit na Sikuwahi kuipeleka kwenye Media Yoyote, Baada ya Ngoma Kuhit ndio Show zikaanza kuja Na Kupata Mshiko".
.
Kwenye Interview Aliyoifanya Na Kipindi Cha #TheClassic Ya E-fm na Mtangazaji Jabir Saleh aka #Kuvichaka, Msanii Wa Muziki Wa Hip Hop Kutoka Hapa Nchini Mr.Blue Byser Amefunguka Hayo Juni 24,2023.
.
Blue Pia Amesema Single Hiyo Ya Pesa imeokoa Maisha Yake Kwa Asilimia 100 Kutoka alipokuwa Chini Mpaka Kwenda Juu Mara Baada ya Kufanya Vizuri Ndani Na Nje Ya Bongo.
#JordanMediaEntUpdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

