CGP NYAMKA AZINDUA MAGARI MAPYA 12 YA JESHI LA MAGEREZA
KAMISHNA Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP) Mzee Ramadhani Nyamka Leo Juni 22,2023 amezindua Magari mapya 12 ya Jeshi la Magereza ambayo yamepokelewa kutoka kwa Wakala wa Ununuzi wa Serikali (GPSA) kati ya magari 23 ambayo Jeshi la Magereza imeyalipia, na kuyagawa katika Vituo vya Magereza Mikoa ambavyo havikuwa na magari.
Aidha, Nyamka amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan, kwa juhudi zake za kuliwezesha Jeshi la Magereza kupata Vyombo vya Usafiri vya uhakika ili kutekeleza majukumu yake kikamilifu.
Uzinduzi huo umefanyika katika Makao Makuu ya Jeshi la Magereza eneo la Msalato jijini Dodoma.
@magerezatanzania
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

