TPA YATAKA TAARIFA ILIYOSAMBAA MITANDAONI KUHUSU BANDARI YA DSM IPUUZWE
MAMLAKA Ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) inapenda Kuwajulisha wateja, Wadau Wa Kitaifa na Kimataifa Na Umma Kwa Ujumla Kwamba, Taarifa zilizosambaa ikisema "Serikali imepanga kuipa Kampuni Ya DP World ya Falme za Dubai Kandarasi ya Uendeshaji Wa Shughuli za Bandari ya Dar es Salaam Kwa muda Wa Miaka 100" hizo Sio Sahihi Na Ni upotoshaji wa Makusudi unaofanywa na Watu Wenye Nia Ovu ya Kukwamisha Mipango thabiti ya Nchi Katika Kuongeza Ufanisi Wa Sekta ya Bandari Ya Nchini Kwa Maslahi Mapana Ya Taifa.
.
TPA imesema Azimio la Bunge linahusu Mkataba Ambao Serikali ya Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania inaingia Na Serikali Ya Dubai wenye ukomo Wa Miezi Kumi Na Mbili (12) Kwa Ajili Ya Kutoa Nafasi Ya Serikali Ya Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania Kujadiliana Na Serikali ya Dubai Kuhusu Maeneo ambayo Serikali Hizo Mbili zinaweza Kushirikiana Katika uboreshaji na uendelezaji Wa Sekta Ya Bandari Nchini Tanzania.
.
Mamlaka Hiyo pia imesema Ushirikiano Wa Nchi Mbili za Dubai na Tanzania una Lengo la Kuongeza Ufanisi Wa Huduma za Bandari Nchini, kukuza Ajira za Watanzania na Kufungua Fursa za Kiuchumi na kijamii Kupitia Uwekezaji Kwenye Baadhi Ya Maeneo Ya Bandari Ya Dar es Salaam, Maeneo huru ya Kiuchumi na Viwanda (Special Economic And Industrial Zone) Kwa Kujenga Viwanda Pamoja Na Uwekezaji Katika Mnyororo mzima Wa Usafirishaji Kutoka Bandari za Tanzania kwenda Nchi za Jirani ambazo zinatumia Bandari Zetu.
.
Aidha, TPA imewaomba Wateja,Wadau na Umma kutambua Kwamba, Jitihada zote na Hatua zilizochukuliwa na Serikali Ya Awamu Ya Sita Katika Kuvutia uwekezaji Nchini Hususani kwenye Maeneo ya Bandari, zinalenga kumaliza Changamoto za muda Mrefu Ikiwemo ucheleweshwaji Wa Meli, Mizigo na kukosekana Kwa Ufanisi Katika Bandari Zetu.
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

