WALIMU ZAIDI YA 500 WAPEWA MAFUNZO MATUMIZI YA VISHIKWAMBI
WALIMU zaidi ya 500 wa shule za sekondari nchini wameanza kupatiwa mafunzo ya matumizi sahihi ya Tehama na Vishkwambi ili kupata mbinu mpya za kufundishia.
Mafunzo hayo yamekuja ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Rais Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa siku ya Mei Mosi 2023 baada ya kusoma moja ya bango la walimu walioomba kupatiwa mafunzo ya jinsi ya kutumia vishkwambi kufundishia.
Akifungua mafunzo hayo mkoani Arusha, Naibu katibu mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Franklin Rwezimula amesema mafunzo hayo ya siku tano yanalenga kuwafundisha walimu 1500 walioko kazini mbinu mpya za matumizi ya TEHAMA na vishkwambi katika kufundishia na kujifunza ili nao wakafundishe wenzao.
"Mafunzo haya yako chini ya mradi wa miaka mitano unaolenga 'kuboresha mazingira ya ujifunzaji, ufundishaji kwenye shule zetu za sekondari' (SEQUIP) , ikiwa ni utekelezaji wa mapinduzi makubwa ya Elimu"
Rwezimula aliwataka walimu hao kuwa makini katika mafunzo ili yakalete tija na wakawe mabalozi wazuri kwenye maeneo yao ya kazi.
"Dunia imezama kwenye Sayansi na Teknolojia, hivyo wizara inategemea kuwanoa ninyi ili muenende na mabadiliko hayo, hivyo basi na nyie bebeni dhamana ya kwenda kuwasaidia wenzenu"
kwa upande wake Mratibu wa SEQUIP, Dkt Mollel Meigaru alisema kuwa Mafunzo hayo yanayolenga kuimarisha Elimu ya sekondari nchini chini ya ufadhili wa benki ya dunia kwa mkopo wa dola milioni 500.
"Mbali na mafunzo haya, pia mradi umefanikisha kutoa mafunzo kwa walimu 18,000 juu ya namna bora ya kufundisha masomo ya sayansi, na kuhusisha na tehama, lakini pia unalenga kujenga miundo mbinu kwa shule za sekondari ambapo unajenga shule 1000 za mchanganyiko na zingine 26 za wasichana kila mkoa"alisema
Alisema mafunzo hayo kwa walimu yanatarajia kuongeza ufaulu kwa wanafunzi hasa wa masomo ya Sayansi na kwenda kuwa msaada mkubwa kwa Taifa baadae.
kwa upande wake Mkurugenzi wa Elimu maalum Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt.Magreth Matonya alimewataka walimu wenye mahitaji maalum waliopata nafasi ya kuhudhuria mafunzo hayo wakawe wakufunzi wazuri.
@wizara_elimutanzania
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

