JKT YATOA WITO KWA WAHITIMU WA KIDATO CHA SITA 2026 KURIPOTI JUNI 1
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Rajabu Mabele ametoa wito kwa Vijana waliohitimu elimu ya Sekondari kidato cha sita mwaka 2026 kutoka shule zote Tanzania Bara na Visiwani kuhudhuria Mafunzo ya JKT kundi la lazima (Mujibu wa Sheria) kwa mwaka 2026.
Akizungumza na waandishi wa Habari leo tarehe 28 Mei 2026 Makao Makuu ya JKT kwa niaba ya Mkuu wa JKT, Mkuu wa Tawi la Utawala JKT, Brigedia Jenerali Hassan Mabena amesema Vijana hao wanatakiwa kuripoti kwenye kambi mbalimbali kuanzia Juni Mosi 2026 Hadi Juni 07,2026.
Brigedia Jenerali Mabena ameongeza kuwa wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho (Physical Disabilities) watatakiwa kuripoti katika Kambi ya Ruvu JKT iliyopo Mlandizi mkoani Pwani ambayo ina miundombinu ya kuhudumia watu watu hao.
Amesema orodha kamili ya vijana waliochaguliwa, makambi ya JKT waliyopangiwa na mahali yalipo makambi hayo inapatikana katika tovuti ya JKT ambayo ni www.jkt.mil.tz
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

