logo

MWANAMKE AFARIKI BAADA YA KUCHOMWA MOTO KISA TATOO YA RAIS RUTO

Mwanamke raia wa Kenya, Rachel Wandeto, amefariki dunia baada ya kujeruhiwa vibaya kwa moto kufuatia kushambuliwa na watu wasiojulikana, tukio linalodaiwa kuchochewa na yeye kuwa na tatoo inayoonyesha sura ya Rais wa Kenya, William Ruto, sehemu ya mwili wake.

‎.

‎Taarifa zinaeleza kuwa Wandeto alipata majeraha ya moto yaliyokadiriwa kufikia zaidi ya asilimia 70 ya mwili wake.

Baada ya tukio hilo, alipelekwa kwa matibabu katika Kenyatta National Hospital jijini Nairobi, ambako alikuwa akipatiwa matibabu maalum kabla ya kufariki dunia.

Watu waliohusika na tukio hilo bado hawajafahamika, huku mamlaka husika zikiendelea na uchunguzi kubaini waliohusika na sababu halisi za shambulio hilo.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn