logo

CHINA YAPIGA MARUFUKU KUFUKUZA WAFANYAKAZI KWA SABABU YA AI

Mahakama moja nchini China imeweka wazi msimamo wake kuhusu matumizi ya Akili Mnemba (AI) kazini, baada ya kuamua kuwa waajiri hawaruhusiwi kuwafukuza kazi wafanyakazi kwa lengo la kuwabadilisha na teknolojia hiyo kwa sababu za kupunguza gharama tu.

‎.

‎Uamuzi huo umetolewa kufuatia kesi iliyofunguliwa na mfanyakazi wa kampuni ya teknolojia aliyelalamika baada ya majukumu yake kuhamishiwa kwenye mfumo wa AI.

‎.

‎Kampuni ilijaribu kumpangia kazi nyingine zenye mshahara mdogo sana, na hatimaye kumfukuza kazi alipokataa mabadiliko hayo.

‎.

‎Mahakama imeamua kuwa hatua hiyo ilikuwa kinyume cha sheria, ikisisitiza kuwa uamuzi wa kampuni kutumia AI ni wa kibiashara, lakini hauwezi kutumika kama sababu halali ya kusitisha ajira bila kuzingatia taratibu stahiki na maslahi ya mfanyakazi.

‎.

‎Aidha, mahakama imesisitiza wajibu wa waajiri kuhakikisha wanatoa mafunzo mapya (retraining) au kuwatafutia wafanyakazi majukumu mbadala yanayokubalika badala ya kuwaondoa kazini moja kwa moja pindi teknolojia mpya inapochukua nafasi ya kazi zao.

‎.

‎Uamuzi huo unatoa ujumbe muhimu kwamba pamoja na kasi ya ukuaji wa AI duniani, haki na ustawi wa binadamu kazini bado vina thamani kubwa kisheria na kijamii.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn