logo

YANGA SC YAPEWA ZAWADI YA SHILING MILIONI 20

WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt.Pindi Chana (@pindi.chana) leo Mei 28, 2023 amewaongoza baadhi ya viongozi wa Serikali, Klabu ya Yanga na mashabiki wa mpira wa miguu kushuhudia mchezo wa kwanza wa Fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika kati ya Dar es Salaam Young Africa (Yanga) dhidi ya USM Alger ya nchini Algeria, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam.

Mchezo huo umemalizika kwa USM Alger kupata ushindi wa magoli 2 kwa 1, ambapo Klabu ya Yanga imepata zawadi ya shilingi Milioni 20 ikiwa ni zawadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa timu hiyo.

@wizara_sanaatz

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn