logo

SMZ KUUNGA MKONO MFUKO WA UPANDIKIZAJI FIGO NA ULOTO BMH

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imeahidi kuunga mkono mfuko maalum wa kuwezesha matibabu ya upandikizaji figo na uloto katika Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) iliyopo jijini Dodoma, ambao unaolenga kusaidia wagonjwa wanaohitaji matibabu hayo.

‎.

‎Mkurugenzi Mtendaji wa BMH, Prof. Abel Makubi, ameyasema hayo wakati wa Uzinduzi wa kilele cha Maadhimisho ya miaka 10 ya hospitali hiyo pamoja na uzinduzi wa mfuko maalum wa kuwezesha matibabu ya upandikizaji figo na uloto, jijini Dodoma.

‎Amesema ahadi hiyo imekuja kufuatia kikao kati ya uongozi wa BMH ukiongozwa na Prof. Makubi na viongozi wa juu wa Zanzibar, akiwemo Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi, pamoja na Makamu wa Pili wa Rais, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla.

‎Amebainisha kuwa uchangiaji wa mfuko huo maalum wa kusaidia matibabu ya wagonjwa 100 wanaohitaji upandikizaji uloto na figo utafanyika tarehe 11 Aprili, 2026 visiwani Zanzibar.

Prof. Makubi ametoa wito kwa taasisi za serikali, sekta binafsi na watu binafsi waliopo Zanzibar kujitokeza kwa wingi kuchangia mfuko huo ili kuokoa maisha ya Watanzania wenye changamoto za ugonjwa wa seli mundu na figo.

BMH ndiyo hospitali pekee katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati inayotoa matibabu ya ugonjwa wa seli mundu kupitia huduma ya upandikizaji uloto.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn