KONDOMU ZA BURE ZAMALIZIKA NDANI YA SIKU 3 OLIMPIKI YA MAJIRA YA BARIDI
Mipira ya kondomu ya bure iliyotolewa kwa wanariadha katika Olimpiki ya Majira ya Baridi imeisha ndani ya siku tatu pekee tangu kuanza kwa mashindano hayo, kwa mujibu wa gazeti la Italia La Stampa.
Kondomu elfu kadhaa zenye nembo ya Olimpiki zilisambazwa kwa washindani waliokuwa wakiishi katika kijiji cha wanamichezo huko Cortina d'Ampezzo nchini Italy.
.
Hata hivyo, mwanariadha mmoja ambaye hakutaka kutajwa jina alinukuliwa akisema kuwa shehena hiyo iliisha haraka kuliko ilivyotarajiwa.
“Ziliisha ndani ya siku tatu tu. Tuliambiwa zitaongezwa zaidi, lakini hadi sasa hakuna anayejua zitafika lini,” alisema.
Utaratibu wa kugawa kondomu bure kwa wanariadha ulianza tangu Olimpiki ya Seoul 1988 kwa lengo la kuongeza uelewa kuhusu kinga dhidi ya maambukizi ya magonjwa ya zinaa.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, idadi ya kondomu zilizotolewa katika Michezo ya Majira ya Baridi ni ndogo ikilinganishwa na Olimpiki ya Paris 2024, ambapo jumla ya kondomu 300,000 zilisambazwa sawa na wastani wa mbili kwa siku kwa kila mwanariadha.
Katika mashindano ya Majira ya Baridi, wanariadha wapatao 3,000 wanashiriki, huku Paris 2024 ikiwa na takribani washiriki 10,500.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

