logo

BAJETI 2026/27 KUAKISI UTEKELEZAJI SERA NA MIPANGO YA ELIMU TANZANIA

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda, leo Februari 12, 2026, amefungua rasmi Baraza la Wafanyakazi la 36 la Wizara hiyo jijini Dodoma.

‎Akizungumza wakati wa ufunguzi huo, Prof. Mkenda aliwapongeza viongozi na watumishi wa wizara kwa juhudi zao katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali, huku akisisitiza umuhimu wa kuongeza kasi ya kutekeleza mipango iliyopangwa ili kufikia malengo ya sekta ya elimu.

‎Aidha, ameelekeza kuwa mipango na makadirio ya Bajeti ya mwaka 2026/27 lazima yaakisi utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 (Toleo la 2023).

Alibainisha maeneo ya kupewa kipaumbele kuwa ni pamoja na elimu ya lazima kwa miaka 10, mpango wa kisayansi wa kujenga umahiri wa kusoma, kuandika na kuhesabu kwa watoto wa elimu ya awali pamoja na wanafunzi wa darasa la kwanza na pili, na kuimarisha mpango wa ushirikiano kati ya vyuo na viwanda.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn