logo

RAIS FAYE ATANGAZA SIKUKUU BAADA YA SENEGAL KUTWAA AFCON NCHINI MOROCCO

Rais wa Senegal, Bassirou Diomaye Faye, ametangaza leo Jumatatu, Januari 19, 2026 kuwa siku ya mapumziko ya kulipwa, kufuatia ushindi wa kihistoria wa timu ya taifa ya soka ya nchi hiyo katika fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).

Simba wa Teranga walitwaa taji hilo la bara Jumapili baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1–0 dhidi ya wenyeji Morocco, katika mchezo uliochezwa mjini Rabat.

Bao pekee la ushindi lilifungwa na Pape Gueye katika muda wa ziada wa dakika za lala salama.

‎Akihutubia taifa kupitia televisheni, Rais Faye amesema uamuzi wa kutangaza siku ya mapumziko unalenga kuwapa wananchi fursa ya kusherehekea kwa pamoja ushindi huo mkubwa na kushiriki furaha ya mafanikio ya timu ya taifa.

‎Mamilioni ya raia wa Senegal wanatarajiwa kufurahia siku hiyo ya mapumziko yenye malipo, huku sherehe kubwa zikitarajiwa kufanyika katika mji mkuu Dakar na miji mingine mikubwa nchini humo.

‎Ushindi huo umeifanya Senegal kutwaa taji la pili la AFCON katika historia yake, na kuzua shangwe kubwa kote nchini, huku mashabiki wakifurika barabarani na maeneo ya umma kuwaenzi wachezaji pamoja na benchi la ufundi.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn