CCM YAZINDUA ZIARA YA KITAIFA NCHI NZIMA
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeendelea kudhihirisha kwa vitendo kuwa ni chama cha wananchi, baada ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) anayeshughulikia Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Ndg. Kenani Labani Kihongosi, kutangaza kuanza kwa ziara ya kitaifa ya kichama itakayofanyika katika mikoa yote ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari leo katika Ukumbi wa Jakaya Convention Centre jijini Dodoma, Ndg. Kihongosi amesema ziara hiyo inalenga kuimarisha ushirikiano kati ya chama, wanachama na wananchi kwa ajili ya kulinda amani, umoja na maendeleo ya Taifa.
.
"Ziara itahusisha kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo pamoja na kusikiliza na kutatua kero za wananchi moja kwa moja.
.
"CCM ina wajibu wa kuisimamia Serikali kwa karibu kwa kushuka kwa wananchi badala ya kutegemea taarifa za mezani pekee,chama kitaendelea kusikiliza changamoto za wananchi na kuchukua hatua stahiki ili kuboresha ustawi wao" alisema Kihongosi.
Ndg. Kihongosi ameongeza kuwa CCM ni chama cha kimaendeleo na kijamii kinachojengwa juu ya misingi ya amani, umoja, mshikamano na kulinda utu wa Mtanzania.
.
Alibainisha kuwa misingi hiyo ndiyo imekiwezesha chama kuiongoza nchi kwa muda mrefu kwa uthabiti na amani, huku kikitanguliza maslahi ya Taifa mbele ya maslahi binafsi au ya makundi.
Vilevile, Mjumbe wa NEC ameipongeza Serikali chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kufanya kikao cha kufungua mwaka na Mabalozi wa Tanzania kutoka nchi mbalimbali, akisema hatua hiyo imeongeza heshima ya Taifa kimataifa na kuwapa faraja wanachama wa CCM kote nchini.
Ameeleza kuwa kupitia ziara hiyo, CCM itatathmini utekelezaji wa ahadi za siku 100 za Rais na kuhakikisha maslahi ya wananchi yanalindwa na hayapotoshwi kwa namna yoyote.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

