FUNKY MATAS AWEKA REKODI YA DUNIA KWA KUWA NA TATTOO 273
Msanii wa tatoo Funky Matas, ameweka Rekodi ya Dunia ya Guinness kwa kuwa na idadi kubwa zaidi ya saini zilizochorwa mwilini kwa mwanaume, akiwa na jumla ya tatoo 273 mgongoni.
.
Miongoni mwa waliotia saini kwenye mwili wake ni nyota wakubwa kama 50 Cent, Kelly Clarkson, Bad Bunny, Samuel L. Jackson, na Usain ..
Mradi huo ulianza kama wazo dogo la kibinafsi kati ya yeye na marafiki, lakini baadaye ukawa safari ya kipekee ya kusherehekea upendo, ushirikishwaji na msukumo.
.
Funky huchagua kwa makini watu ambao wametoa mchango chanya katika maisha yake, na kila sahihi hubadilishwa kuwa tatoo mara moja au muda mfupi baada ya kutiwa.
Ingawa hakuwahi kupanga kuvunja rekodi, safari yake sasa imegeuka kuwa kielelezo chenye thamani cha uhusiano, kumbukumbu na furaha.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

