logo

MWANZA YAKUSANYA MAPATO SHILINGI BILIONI 216.2 KATIKA KIPINDI CHA MIAKA 5 YA SERIKALI YA RAIS DKT.SAMIA

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Said Mtanda, amesema makusanyo ya mapato ya ndani kwenye Halmashauri yameongezeka kutoka jumla ya Shilingi Bilioni 44.2 mwaka 2020/21 hadi Shilingi Bilioni 70.7 mwaka 2024/25 kufikia mwezi Mei, 2025 sawa na ongezeko la asilimia 60.

‎.

‎"Aidha, kwa kipindi cha miaka mitano (5) zimekusanywa jumla ya Shilingi Bilioni 216.2" alisema.

‎.

‎Mhe. Mtanda ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Watanzania kupitia mkutano na Waandishi wa Habari kuhusu mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita katika mkoa huo leo Julai 16,2025 katika Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo) jijini Dodoma.

‎.

‎Amesema mapato ya Hifadhi ya Taifa ya Saanane yatokanayo na Utalii yameongezeka kutoka Shilingi 210,818,714.53 mwaka 2020 hadi Shilingi 274,488,877.09 mwaka 2025 sawa na ongezeko la Shilingi 63,670,162.56.

‎.

‎"Idadi ya watalii waliotembelea Hifadhi ya Taifa ya Saanane imeongezeka kutoka 13,175 mwaka 2020 hadi 24,748 mwaka 2025 sawa na ongezeko la watalii 11,573." alisema Mtanda.

‎.

Mtanda amesema Ufugaji wa samaki kwa kutumia njia ya kisasa umeongezeka kutoka vizimba (fish cauges) 1,664 mwaka 2020 hadi 2,715 mwaka 2025 sawa na ongezeko la vizimba 1,051, huku Jumla ya tani 43,657.6 za minofu ya Samaki zimechakatwa na tani 81,812 zimesafirishwa kwenda soko la nje ya Nchi kupitia Uwanja wa Ndege wa Mwanza.

‎.

‎Aidha, Mtanda amesema uzalishaji wa mazao ya chakula umeongezeka kutoka tani 640,205.3 (37.59%) 2020/21 hadi kufikia tani 1,025,784.08 (60.23%) mwaka 2024/25 sawa na ongezeko la Tani 385,578 (22.64%).

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn