logo

TRA SINGIDA YAKUSANYA SHILINGI ‎BILIONI 30 MWAKA 2024/25

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe. Halima Dendego, amesema katika kipindi cha miaka mitano (5) ya Serikali ya Awamu ya Sita, makusanyo ya TRA mkoani humo yameongezeka kutoka shilingi Bilioni 11.9 mwaka 2021/22 hadi Shilingi Bilioni 30 mwaka 2024/25 sawa na asilimia 152.

‎.

‎"Makusanyo ya mapato ya ndani yameongezeka kutoka Shilingi Bilioni 14.6 mwaka 2020/21 hadi Shilingi Bilioni 24.8 mwaka 2024/25 sawa na asilimia 69.8" alisema.

‎.

‎Mhe. Dendego ameyasema hayo leo Julai 04,2025 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita katika mkoa huo katika Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo) jijini Dodoma.

‎.

‎Amesema Upatikanaji wa maji safi mjini, mkoa wa Singida umefikia asilimia 77.6 kutoka asilimia 53.33 mwaka 2021/22 na vijijini wamefikia asilimia 70 kutoka asilimia 57.9 mwaka 2021/22.

‎.

‎"Upatikanaji wa maji katika miji midogo ya Manispaa, Ikungi, Iguguno, Puma umefikia 86%. Ujenzi wa bwawa la maji taka umefikia 70%" alisema Dendego.

‎.

‎Kwa upande mwingine, Mhe. Dendego amesema kumekuwa na ongezeko la vituo vya kutolea huduma za Afya kuanzia ngazi ya Zahanati hadi Hospitali kutoka vituo 203 mwaka 2020/21

‎hadi vituo 302 mwaka 2024/25.

‎.

‎Aidha, Mhe. Dendego amesema Usajili wa wakulima umeongezeka kutoka wakulima 75,398 mwaka 2020/21 hadi wakulima 293,385 mwaka 2024/25 sawa na 289%.

‎.

‎"Matumizi ya mbolea yameongezeka kutoka tani 1,772.5 mwaka 2021/22 hadi tani 7,948.75 mwaka 2024/25 sawa na 348.4%. Matumizi ya mbegu bora yameongezeka kutoka tani 625.5 mwaka 2020/21 hadi tani 1,397.2 mwaka 2024/25 sawa na 123.4%" alisema Dendego.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn