NAIBU KATIBU MKUU MPYA ELIMU DKT. HUSSEIN OMAR APOKELEWA RASMI WIZARANI
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo, leo Juni 27, 2025 amempokea rasmi Naibu Katibu Mkuu mpya anayeshughulikia Elimu, Dkt. Hussein Mohamed Omar, katika hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
Katika hotuba yake ya kumkaribisha, Prof. Nombo alieleza kuwa Wizara inaendelea kutekeleza mageuzi makubwa ya elimu yanayolenga kutoa stadi, maarifa, na ujuzi kwa Watanzania. Alimhakikishia Dkt. Omar ushirikiano wa karibu katika kuhakikisha dira hiyo inatekelezwa kikamilifu.
Kwa upande wake, Dkt. Omar ametoa shukrani kwa mapokezi mazuri aliyoyapata kutoka kwa watumishi wa Wizara, na akasisitiza kuwa yupo tayari kuwajibika ipasavyo katika kuendeleza mageuzi ya elimu katika nyanja zote.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

