WAZIRI MKENDA :VITIMWENDO 253 TUMENUNUA KWA WANAFUNZI 253 WENYE MAHITAJI MAALUM
"SERIKALI imenunua na kusambaza vitimwendo 253 kwa wanafunzi wa shule za msingi 200 na sekondari 53 wenye mahitaji maalum kwa lengo la kuwawezesha kumudu mazingira ya shule na nyumbani, imenunua vifaa saidizi vya kuongeza usikivu 100 kwa wanafunzi wa Elimu ya Msingi 30 na Vyuo Vikuu 70 kwa lengo la kuboresha ufundishaji na ujifunzaji".
.
Hayo Yamesemwa Na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda Leo Mei 16, 2023 amewasilisha Bungeni Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Wizara kwa Mwaka 2023/24.
.
Mkenda Amesema Serikali imewezesha upatikanaji wa huduma za kujikimu, ada na vifaa wezeshi kwa wanafunzi 130 wenye mahitaji maalum hususani wanaotoka katika mazingira magumu.
.
"Serikali imekamilisha ujenzi na kuzindua Shule za Msingi Jumuishi za mfano moja iliyopo Masasi na nyingine Meru zenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 480 kila Moja" Amesema Mkenda.
.
Waziri Huyo Amesema Serikali imeendelea na uchapaji wa vitabu 2,000,000 vya masomo ya Sayansi na Hisabati kwa ajili ya kusambaza katika Halmashauri zenye upungufu mkubwa.
.
Aidha, Mkenda Amesema Serikali imewezesha upanuzi wa shule kongwe 18 na ukarabati wa shule kongwe 16 za sekondari, imejenga shule ya mfano ya sekondari Dodoma katika eneo la Iyumbu yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 1,000 ambapo ujenzi umefikia asilimia 87, imejenga upya vituo vinne kwa ajili utoaji wa Elimu ya Sekondari Nje ya Mfumo Rasmi na imekarabati vituo 4 vya aina hiyo.
@wizara_elimutanzania
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

