logo

UJENZI UWANJA WA NDEGE SHINYANGA UMEFIKIA ASILIMIA 73.9 -WAZIRI MKUU MAJALIWA

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amemtaka mkandarasi wa ujenzi wa uwanja wa ndege wa Shinyanga afanye kazi usiku na mchana ili kuhakikisha anakamilisha ujenzi wa uwanja huo ikiwemo ufungaji wa taa na uanze kutumika wakati wote.

Amesema kuwa uwanja huo ni wa kimkakati uliokuwa ukisubiriwa kwa muda mrefu na wakazi wa mkoa wa Shinyanga na maeneo ya jirani ikiwemo mkoa wa Simiyu.

Mhe. Majaliwa amesema hayo leo Jumapili (Februari 16, 2025) wakati alipokagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa uwanja wa ndege wa Shinyanga ambao kwa ujumla ujenzi wake umefikia Asilimia 73.9.

CHICO tunajua unafanya kazi nzuri, hapa kasoro yako unachelewesha kuingiza vifaa vilivyobaki, Meneja wa TANROADS ameniambia mmekamilisha kwa asilimia 100 kwenye eneo la kuruka na kutua ndege, sio kweli, bado taa, kwahiyo agiza taa mara moja zije hapa, tunaweza kuutumia uwanja wetu usiku, hata kama jengo halijakamilika, mnaweza kutumia jengo la zamani, hamdai chochote fedha zote mmelipwa” alisema.

Amesema kuwa dhamira ya Serikali ya kuendelea kuimarisha Sekta ya usafirishaji ni dhamira kamili na kwa sasa inatekelezwa kwa vitendo.

.

Aidha, Mheshimiwa Majaliwa amewataka Watanzania waliofanya kazi za ujenzi kwenye uwanja wa ndege wa Shinyanga kutumia uzoefu na ujuzi walioupata kujiendeleza na ikiwezekana kuanzisha makampuni ya ujenzi ili kunufaika na miradi mingine itakayotolewa na Serikali.

Naye, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi amemshukuru Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika mkoa huo ikiwemo ujenzi wa uwanja wa ndege.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn