VIJANA WENYE USONJI HAWAJAACHWA NYUMA KWENYE SERA MPYA YA ELIMU- RIDHIWANI KIKWETE
Waziri Wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana,Ajira na wenye Ulemavu Mhe.Ridhiwani Kikwete amewataka watendaji wa Wizara ya Elimu kuliangalia eneo la Ushindani uliopo na utekelezaji wa Sera mpya ya Elimu ujikite katika kutatua changamoto zilizopo nchini.
.
Ridhiwani ameyasema hayo leo Februari 11,2025 alipokuwa akimwakilisha Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda kwenye kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake Na Wasichana katika Sayansi tukio lililofanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Center Jijini Dodoma.
.
Amesema Serikali inaendelea kutambua changamoto ya Usonji katika jamii yetu, na katika kufanya hilo kupitia Sera Mpya ya Elimu, vijana wenye changamoto ya Usonji ambao ndani yao wana kipaji maalum nalo pia limeangaliwa.
.
"Tunacho chuo cha Patandi ambacho chuo hicho kinaendelea kuwaangalia na kuwafundisha walimu na kukuza vipaji Vya Vijana wenye Usonji, hivyo jambo hilo halijaachwa nyuma" alisema Waziri Ridhiwani.
.
Waziri Ridhiwani amesema kundi la Wanawake na Wasichana ni kundi ambalo takribani linatengeneza asilimia 49.7 ya watu wote duniani, kwa mujibu Wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 kwa Tanzania, Wanawake na Wasichana ni Asilimia 51.3.
.
"Kiwango Cha Wanawake na Wasichana wanaoshiriki kwenye nyanja za kazi za STEM duniani zinakadiriwa kuwa Asilimia 33 pekee" alisema.
.
Aidha, Ridhiwani amesema tunapowawezesha Wasichana na Wanawake katika kushiriki Katika Sayansi na Uongozi, Sio tu tutaimarisha Usawa wa Kijinsia bali pia tutazidi kuimarisha utafiti ubunifu unaojibu changamoto na mahitaji ya kiuchumi na kijamii nchini na kwingineko.
.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu,Utamaduni na Michezo Ndg. Musa Ramadhani Sima (Mb) amesema kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya awamu ya sita ni kuwafanya vijana wawe na ujuzi, na mpaka hivi Sasa Serikali imeshaanzisha Elimu ya Amali,Vyuo vingi Vya VETA nk.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

