MUHIMBILI MLOGANZILA YAANZISHWA HUDUMA YA KUJIFUNGULIA KWENYE JAKUZI
Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila imeanzisha huduma ya kinamama wajawazito kujifungulia katika jakuzi maalum (water birth), huduma ambayo inamsaidia mama kupunguza uchungu na kumuepusha kuchanika wakati wa kujifungua.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga, Dkt. Debora Bukuku kuanzishwa kwa huduma hiyo ni mwendelezo wa kupanua wigo wa huduma kwakuwa awali katika Hospitali za Umma huduma hizo zilikuwa zinapatikana Muhimbili Upanga pekee .
Kwa upande wake Muuguzi Mkunga Bingwa na Mtaalam wa kusaidia kinamama kujifungulia kwenye jakuzi Bw. Rwehabura France amesema miongoni mwa faida za mama kujifungulia kwenye jakuzi ni pamoja kupata fursa ya kukaa na wataalam na ndugu atayemchagua kukaa naye kwa muda wote atakaokuwa kwenye jakuzi kitu ambacho kitamuongezea faraja zaidi na kutohisi maumivu.
Bw. France ameongeza kuwa kabla ya mama kupatiwa huduma hiyo huwa anapatiwa elimu kuhusu mtiririko wa huduma hiyo ambapo pia amebainisha kuwa huduma hiyo ni salama kwa mama na mtoto atakayezaliwa.
Kwa upande mama aliyejifungulia kwenye jakuzi hospitalini hapo Bi. Rahel Mushi amesema amefurahishwa na huduma hiyo kwakuwa wataalam walikuwa wanampatia mazoezi wakati wote akiwa kwenye jakuzi na kumfanya asihisi maumivu, hivyo anawashauri wakina mama wengine kutumia huduma hiyo.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

