DKT.BITEKO: UWEZO WA TANZANIA KUZALISHA UMEME UTAONGEZEKA HADI MEGAWATI 4,000 MWISHONI MWA MWAKA 2025
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema Ifikapo mwisho wa mwaka 2025, uwezo wa Tanzania kuzalisha umeme utaongezeka hadi kufikia megawati 4,000.
.
"Nishati yetu inatoka kwenye vyanzo safi na mbadala vinavyonufaisha wakazi wa vijijini na mijini, huku miundombinu ya umeme ikifikia vijiji vyote 12,318 nchini" alisema Dkt.Biteko.
.
Dkt. Biteko ameyasema hayo alipokuwa akifungua mkutano wa Kimataifa wa Nishati unaowakutanisha Viongozi mbalimbali wa Afrika, Mashirika ya Kimataifa; Viongozi wa Benki ya Dunia, Benki ya Maendeleo ya Afrika na taasisi ya Rockefeller (M300) unayofanyika leo Januari 27,2025 jijini Dar es salaam.
Amesema baada ya kupata Uhuru mwaka 1960, nchi za Afrika zimepiga hatua kubwa katika kuzalisha na kusambaza umeme kwa wananchi wao.
.
"Tanzania ilikuwa na uwezo wa kuzalisha megawati 21 pekee wakati wa Uhuru, kwa sasa nchi ina uwezo wa kuzalisha megawati 3,160" alisema Dkt.Biteko.
.
Naibu Waziri Mkuu amesema pamoja na mafanikio makubwa ya kuzalisha umeme barani Afrika, takribani Waafrika milioni 571 bado hawana huduma ya umeme, hivyo mkutano huo umeitishwa rasmi kwa lengo la kujadili namna ya kuongeza upatikanaji wa umeme kwa watu milioni 300 barani Afrika katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
.
Aidha,Dkt. Biteko amesema Tanzania inaimarisha muunganiko wa Afrika kwani ina miundombinu ya umeme inayounganisha nchi za Kenya, Burundi, Rwanda, na Uganda, huku miundombinu ya kuunganisha Zambia ikiwa inaendelea.
.
Naye Rais wa Benki ya Dunia (WB), Bw. Ajay Banga amesema tunaweza kubadilisha sura ya Afrika kwa kuwa na juhudi za pamoja za kuunganisha rasilimali zilizopo kuhakikisha nishati ya umeme inawafikia wananchi wengi zaidi Afrika ifikapo 2030.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

