logo

WAZIRI MKENDA AMESEMA SERIKALI INAKWENDA KUFUFUA SHULE ZA SEKONDARI ZA UFUNDI

WAZIRI Wa Elimu, Sayansi Na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda Amesema Serikali imekusudia kufufua na kurudisha Shule za Sekondari na Ufundi ambazo zitaanza kuchukua wanafunzi kuanzia Mwezi Januari 2024.
.
"Tunakwenda Kuzifufua Shule za Ufundi Na Yatakuwa Ni Mafunzo Ya Amali Yenye Muelekeo Wa Uhandisi. Shule zenyewe Ifunda Tech, Iyunga Tech,Tanga Tech, Chato Tech, Iyunga Tech,Bwiru Boys, Musoma Tech, Moshi Tech, Mwadui Tech Na Mtwara Tech".

Mkenda Ameyasema hayo Leo Mei 12,2023 Alipokuwa Akifungua Kongamano la Sera na Mitaala ya Elimu Katika Ukumbi Wa Jakaya Kikwete Convertion Center Jijini Dodoma.
.
Amesema mapendekezo ya kufufua shule za sekondari za ufundi ni kutokana na vijana wengi kuona kama kusoma ufundi bila kuwa na elimu ya sekondari ni kujidhalilisha .

“Tumetenga bajeti ya kurudisha shule zetu za sekondari ambazo pia zinafundisha masomo ya ufundi ,hii ni kwa sababu tumeona vijana wengi wakienda kusoma katika vyuo vya ufundi,wanarudi tena kufanya Mtihani wa kidato cha sita ili waende vyuo vikuu,wakidhani kusoma ufundi ni kujidhalilisha.” Alisema Mkenda.
.
Waziri Huyo amesema katika Mapendekezo ya Sera Mpya ya Elimu na Mitaala, serikali imependekeza elimu ya msingi iwe kwa kipindi cha miaka 6 badala ya Saba lakini pia mwanafunzi lazima asome Shule ya Msingi na Sekondari (O-Level).

Aidha, Mkenda Amesema kuhusu namna ya kupata walimu aliwatoa wasiwasi walimu waliopo kazini huku akisema utaratibu huo hautawahusu.

“Niwatoe hofu walimu waliopo kazini,tutakapoanza utaratibu mpya wa kupata walimu ,wao hautawahusu na wataendelea na kazi mpaka watakapostaafu na badala yake Serikali itaangalia namna ya kuwapa nafasi ya kwenda kujiendeleza kielimu.” Amesema Mkenda.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof. Caroline Nombo amesema Katika utekelezaji wa Rasimu hiyo kulikuwa na kamati mbili ambazo zimefanya kazi ya kukusanya maoni ambapo zaidi ya wadau 200,000 walifikiwa na kupata fursa ya kutoa maoni yao kuhusu maboresho ya Sera na Mitaala ya elimu hapa Nchini.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn