
SHEMDOE: MTU MMOJA ANAPASWA KUNYWA MAZIWA LITA 200 KWA MWAKA
KWA Mujibu Wa Shirika La Chakula Duniani Mtu Mmoja anatakiwa kunywa Maziwa Lita 200 Kwa Mwaka Lakini Kwa Hapa Nchini Wastani Wa Unywaji Wa Maziwa Ni Lita 62 Kwa Mtu Kwa Mwaka.
.
Hayo Yamesemwa Na Katibu Mkuu Wa wizara Ya Mifugo Na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe Leo Mei 11,2023 Jijini Dodoma Alipokuwa Akifungua Kikao Cha Mpango Wa Unywaji Maziwa Shuleni Katika Ukumbi Wa Hoteli Ya Royal Village.
.
Shemdoe Amesema Bado Tupo Chini Sana na Kama Wizara Ya Mifugo Na Uvuvi wameona Ni Vyema Kuona Namna Gani Wana Mpango Maalum Wa Kuhakikisha ya Kwamba Watoto waliopo Mashuleni wanaweza Kupata Maziwa.
.
"Tuko Na Wadau Lakini Pia kama Serikali, Wadau Wa Maendeleo Na Sekta Binafsi Ili Hasa wale wazalishaji Wa Maziwa waweze Kuona ni Mahali na Wenyewe wanaweza Kuchangia kwenye Suala Hilo la Unywaji Wa Maziwa.
.
"Tuna Viwanda vinazalisha Maziwa Ambavyo vinachakata Maziwa Ambavyo vimetusapoti kwenye Shule 134 ambapo tuna Shule 130 za Msingi Na Shule 4 Za Sekondari Wadau wameweza kutusaidia Kuendeleza Programu Hiyo" Amesema Shemdoe.
.
Amesema Program Hiyo Wanaiandalia Mpango Mkakati Ambao Utasaidia Wakati watakapoenda Kutekeleza Mahali popote Unywaji Wa Maziwa basi wawe na Kitu kinachowaelekeza.
.
Katibu Mkuu huyo Ametoa Rai Kwa Wadau Wote waweze Kuangalia Mpango Wa Unywaji Maziwa Shuleni na kuuona Namna Gani Kila Mdau anaweza Kuchangia na Kusaidia Serikali Ili waweze Kuongeza Idadi ya Shule.
.
"Hizi Shule 134 ni Chini Ya Asilimia 1& ya Shule Zote tulizonazo. Tungependa Pengine Ndani Ya Miaka 2 ijayo basi Tutoke kwenye Hii Asilimia 1% Mpaka Kufikia Asilimia 20%" Amesema Shemdoe.
.
Aidha, Shemdoe Amesema Wiki Ya Unywaji Wa Maziwa Kwa Mwaka Huu 2023 Itaanza Tarehe 29 Mei Hadi Tarehe 1 Mwezi Juni Na Kitaifa itaadhimishwa Katika Mkoa Wa Tabora.
.
Nae Msajili Wa Bodi Ya Maziwa Tanzania Dkt. George Msalya Amesema Lengo Kubwa La Mpango Huo Ni Kwa Ajili Ya Kupata uendelevu Wa Utoaji Wa Maziwa Mashuleni.
.
Msalya Amewataka Watanzania,Wadau Mbalimbali Na Mashirika ya Kiserikali Kutumia Mpango Huo Kwa Ajili Ya Miradi Endelevu na Program Endelevu Unywaji Wa Maziwa Shuleni.
#JordanMediaupdates
Tranding News

Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news