NMB YASAINI MAKUBALIANO YA MIAKA 3 NA ZIPA
BENKI ya NMB Leo Mei 09,2023 imesaini makubaliano ya miaka mitatu ya ushirikiano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji (ZIPA).
Makubaliano hayo yanalenga Utekelezaji wa awamu ya pili ya kutengeneza mfumo wa kufuatilia taarifa na kuwahudumia wawekezaji Zanzibar, watawezesha uunganishaji wa mfumo wa ZIPA na mifumo ya Idara ya Uhamiaji, Mamlaka ya Mapato na Wakala wa Usajili Mali na Biashara (BPRA).
.
Na Pia Makubaliano hayo Yanalenga Kuendelea kushirikiana katika kutangaza vivutio vya uwekezaji nchini, NMB kutoa suluhishi za kifedha kwa wawekezaji na kutoa suluhishi za ukusanyaji wa mapato kwa njia za kidijitali Na Kushirikiana kwenye matukio muhimu ya kibiashara na kuitangaza nchi.
Makubaliano hayo yamesainiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wetu, Ruth Zaipuna na Mkurugenzi Mtendaji wa ZIPA, Sharif A. Sharif; na kushuhudiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji, Mhe. Mudrick Ramadhan Soraga; Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Serikali Mtandao, Said S. Said; Afisa Mkuu wetu wa Wateja Wakubwa na Serikali, Alfred Shao na viongozi wengine wa Serikali na Benki.
@nmbtanzania
@zipazanzibar
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

