logo

WANANCHI TEMBELEENI HIFADHI ZA BAHARI -HALIMA TOSILI

AFISA Masoko wa Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu nchini Halima Tosili amemshukuru Rais Dkt.Samia kwa maonesho ya wakulima,wafugaji na Wavuvi kwani yanatoa fursa kwa wadau mbalimbali wakiwemo wa Hifadhi za Bahari kutoa elimu kwa wananchi kuhusu rasilimali zilizopo nchini .

Aidha amewaomba wadau na wawekezaji mbalimbali kuwekeza kwenye Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu lakini pia amewasihi wananchi kutembelea maeneo ya hifadhi za bahari kwani kuna vitu vingi vya kujifunza.

Tosili amesema hayo wakati akizungimza na waandidhi wa habari mwishoni mwa wiki wakati wa maonesho hayo yaliyoganyika kitaifa mkoani Dodoma katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.

Alisema katika kuunga mkono Juhudi za Rais Samia katika kuhamasisha utalii na kufikia malengo kwamba ifikapo 2026 Tanzania iweze kufikiwa na watalii milioni tano ,nao wanahamasisha wananchi kufanya utalii wa maeneo ya Bahari .

Alisema wanasimamia hifadhi tatu na maeneo tengefu 15 na kufanya hifadhi za bahari wanazozisimamia kifikia 18.

Alisema hifadhi hizo zimegawanyika katika mikoa minne Tanzania Bara ambazo ni Hifadhi ya kisiwa cha Mafia,Hifadhi za Bahari Dar Es Slaam ,Mnazibay Mtwara na Tanga.

Tosili alisema mwaka huu wameshiriki maonesho ya wakulima,wafugaji na wavuvi kwa lengo la kutoa elimu kwa jamii kuhusiana na suala la uhifadhi wa bahari na umuhimu wa uhifadhi na kuiambia jamii kwamba wao ni moja ya wahifadhi huku akisema fursa hiyo wameitumia kikamilifu kwa watu waliopita kwenye banda lao.

Ametumia fursa hiyo kuwasihi wananchi kutembelea Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu ili ashuhudia rasilimali za bahari zilizopo nchini ili kujionea utalii mbalimbali ukiwemo wa kutembea njia za msituni, kuogelea,kushuhudia magofu ya kale ya kuanzia karne ya 13, lakini pia jamii mbalimbali za kasa,bustani za matumbale,nyangumi wanaohama ,bwawa lenye viboko pamoja na kuona fukwe nzuri zenye mchango mzuri.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn