WATUMIAJI HUDUMA ZA BIMA NCHINI WAMEONGEZEKA HADI KUFIKIA MILIONI 12+ - MENEJA HADIJA MAULID
Meneja wa Uhusiano na Mawasiliano Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania(TIRA) Bi.Hadija Maulid amesema kwa takwimu za mwaka 2021, mpaka hivi sasa watumiaji wa huduma za Bima wameongezeka kutoka milioni 6 hadi kufikia zaidi ya milioni 12, sawa na ongezeko la takribani asilimia 100%.
.
Bi.Hadija ameyasema hayo leo Juni 19,2024 alipokuwa akifanya mahojiano na waandishi wa Habari kwenye ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma katika Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.
.
Aidha,Meneja Hadija ametoa rai kwa wananchi kutumia huduma mbalimbali za Bima ili kuweza kujikinga na majanga ambayo yasiyotarajiwa.
.
"Sisi TIRA tupo na tuna jukumu la kusimamia haki za wateja wa Bima, hivyo popote pale ambapo mteja wa Bima anajikuta amepatwa na changamoto mbalimbali iwe kwenye madai nk. tupo kulisimamia na kuhakikisha kwamba haki zake za msingi zinapatikana kwa mujibu wa Taratibu husika" alisema Bi.Hadija.
.
Kwa upande wake Meneja wa Usimamizi wa Utekelezaji wa Sheria kutoka mamlaka hiyo Bw.Okoka Mgavilenzi amesema kwa hivi sasa wamepanua wigo wa utoaji huduma zao hapa nchini ambapo wana ofisi za kanda 10, na ofisi hizo zinahudumia wananchi popote pale walipo.
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

