WIZARA TATU (3) KUKUTANA KUJADILI UANZISHWAJI WA SHULE ZA AMALI MICHEZO
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda amesema Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia itakaa na Ofisi ya Rais -TAMISEMI pamoja na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ili kuona namna bora ya kuanzisha shule za amali ya michezo.
Akizungumza Juni 25,2024 Mkoani Tabora wakati wa kifunga Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) ambayo yalianza Juni 5, 2024 amesema kuwa Wizara itaangalia namna ya kila mkoa kuwa na shule ya michezo.
Prof.Mkenda ameongeza kuwa katika shule hizo ambazo zitaanza kuanzia Msingi hadi Kidato cha nne zitakuwa na michezo yote pamoja na miundombinu itakayowezesha wanafunzi kujifunza kwa vitendo.
"Tanzania kwa sasa tunauwqkilishi mdogo katika michezo kimataifa hivyo ni wajibu wa wizara zetu hizi tatu kwa pamoja kushirikiana kutambua vijana wenye vipaji kuanzia mashuleni" amesema Mkenda.
Kiongozi huyo ameongeza kuwa ili kuwa na wanamichezo mahiri na wenye uwezo wa kushiriki katika mashindano ya kimataifa ni lazima kuhakikisha watoto wanajifunza michezo kutoka shule za msingi.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news