DUWASA WEKENI ULINZI MAENEO YA MABWAWA YA MAJITAKA - WAZIRI JAFO
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira na Muungano) Mhe. Dkt. Selemani Jafo ameitaka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) kuweka ulinzi katika maeneo ya mabwawa ya Majitaka ili kuzuia uvamizi wa maeneo hayo.
Mhe.Dkt.Jafo ameyasema hayo Juni 4, 2024 wakati alipotembelea Banda la Maonesho la DUWASA katika Maonyesho ya Wiki ya Mazingira Duniani yanayofanyika katika Viwanja vya Jakaya Kikwete Jijini Dodoma,ambayo kilele chake ni Juni 05, 2024.
Amesema madhara ya watu kuvamia maeneo hayo kutasababisha uharibifu wa mazingira lakini pia ni sehemu ya kulinda afya za wananchi.
Maonesho ya Wiki ya Mazingira yalianza Juni 01,2024 yakiwa na Kauli Mbiu isemayo "Urejeshwaji wa Ardhi, Ustahimilivu wa Hali ya Jangwa na Ukame".
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

