logo

UONGOZI BENJAMIN MKAPA HOSPITAL (BMH)WATUA NCHI ZA EAC

Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH)Dkt.Alphonce Chandika akiambatana na baadhi ya wataalamu kutoka BMH wametembelea baadhi ya nchi wanachama wa Afrika Mashariki (EAC).

"Tumekuja kwa mambo mawili, moja ni kuhudhuria vikao tulivyoalikwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki ambavyo vinalenga kujadiliana uanzishwaji wa Kituo cha Umahiri cha upandikizaji Uloto, pili tumekuja kuitangaza huduma ya upandikizaji Uloto inayotolewa na Hospitali ya Benjamin Mkapa pekee katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati" alisema Dkt.Chandika.

Mkurugenzi Mtendaji pamoja na wataalamu wa BMH wametembelea nchi za Rwanda, Burundi, Kenya na Uganda.

Hospitali ya Benjamin Mkapa imeendelea kuanzisha huduma mpya zitakazo nufaisha watanzania na Afrika kwa ujumla.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn