logo

YONAZI: SIMAMIENI VIZURI MRADI WA KUENDELEZA KILIMO NA UVUVI

KATIBU Mkuu Ofisi Ya Waziri Mkuu Sera, Bunge Na Uratibu Dkt.Jim Yonazi Ametoa Wito Kwa Wakurugenzi Wote Nchini, Makatibu Tawala Kuhakikisha Kwamba Wanasimamia Vizuri Mradi Wa Programu Ya Kuendeleza Kilimo Na Uvuvi Katika Maeneo Yao.

.

"Lakini Pia Maafisa Viungo Ninyi ndio Watendaji wakuu Na Ni watekelezaji kabisa, Kuhakikisha Kwamba Mambo Haya Tunayoyatazamia yanatekelezwa Kwa Uhakika" Amesema Yonazi.

.

Ameyasema Hayo Leo Mei 04,2023 Jijini Dodoma alipokuwa Akifungua Warsha Ya Utambulisho Na Uelewa Wa Programu Kwa Watendaji Wa Mikoa Na Halmashauri.

.

Yonazi Pia Amewaomba watekelezaji Wa Kwenye Taasisi Husika Kuhakikisha Mradi Huo Unafanikiwa Kwa Wakati Pasipo kukwama Njiani.

"Ninyi ni Watekelezaji Wa Kitaalamu, Mmepewa Fedha Hizi Pamoja na Vifaa Ili Kazi Hizi ziweze Kutekelezwa Vizuri" Amesema Yonazi.

Katibu Mkuu Huyo Amesema Programu Hiyo Itawezesha Ujenzi, Ukarabati Na Ukaguzi Wa Miundombinu ya Vituo Vya Kuendeleza Vizazi Vya Viumbe Maji Kama Vile Kinguluwila-Morogoro,Lubambagwe- Geita na Itakarabati Miundombinu ya Mabwawa.

Nae Mkurugenzi Idara Ya Sera, Na Uratibu Wa Shughuli za Serikali Bw. Paul Sangawe Amesema Katika Programu Hiyo wanatazamia Meli zitanunuliwa Kwa Upande Wa Tanzania Bara Na Visiwani zitakazo wezesha Nchi Yetu Kwa mara Ya Kwanza kuweza Kufanya Uvuvi Katika Bahari Kuu Ili kuweza Kutumia Rasilimali ambazo tunazo na Tunaweza kuzitumia Kwa Ufanisi.

.

Sangawe Amesema Lengo Kubwa la Mkutano Huo Ni Kuitambulisha Programu Ili kuweza Kujua Majukumu Yao Na Pia Vile vile waweze Kufuatilia Utekelezaji Wa Programu Kuhakikisha Kwamba Fedha ambazo wamepewa Mkopo Wa Dola Milioni 58.8 zinatumika Kwa Ufanisi.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn