logo

RAJABU AFUNGWA KIFUNGO CHA ‎MAISHA JELA KWA KUSAFIRISHA BANGI KILO 109

Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Morogoro imemhukumu Rajabu Ally Mijinga (42) mkazi wa Nyarutanga, Morogoro, kutumikia kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kusafirisha bangi yenye uzito wa kilogramu 109.

‎Hukumu hiyo ilitolewa Machi 30, 2026 na Jaji Magoiga katika kesi ya Uhujumu Uchumi Na. 2326/2025, chini ya Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya pamoja na Sheria ya Uhujumu Uchumi.

‎.

‎Upande wa mashitaka ulithibitisha kuwa mshtakiwa alikamatwa Agosti 17,2024 eneo la Mafumbo Nyarutanga akiwa na bangi hiyo iliyohifadhiwa katika mifuko mitano ya salfeti.

‎Mahakama iliridhika kuwa ushahidi uliowasilishwa Mahakamani ulikuwa wa kutosha na usioacha shaka.

‎.

‎Aidha, utetezi wa mshtakiwa haukuweza kuibua shaka yoyote dhidi ya ushahidi huo.

“Kwa kuzingatia uzito wa kosa hili na madhara yake kwa jamii, Mahakama inamkuta mshtakiwa na hatia,” alisema Jaji Magoiga.

‎Pamoja na hukumu iliyotelewa, Mahakama imeamuru bangi iliyokamatwa iteketezwe, huku mshtakiwa akiwa na haki ya kukata rufaa kama hajaridhika na hukumu hiyo.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn