logo

PROF.KIPANYULA ATAJA NGUZO KUJENGA NM-AIST BORA

Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof.Maulilio Kipanyula amesema uadilifu na kujitoa ni nguzo katika kutimiza majukumu ya uongozi na kujenga NM-AIST.

Ameyasema hayo Mei 21,2024 Arusha wakati akifungua mafunzo ya siku tano ya Menejimenti na Watafiti yaliyoandaliwa na Taasisi hiyo kwa lengo la kuwajengea uwezo viongozi hao.

Mafunzo hayo yanalenga kuongeza uelewa wa uwajibikaji na uadilifu katika utumishi wa umma, miiko ya uongozi, usimamizi wa fedha za umma ,uandaaji wa bajeti , matumizi ya fedha kudhibiti na kusimamia msongo wa mawazo pamoja na kusimamia afya ya akili.

Mafunzo hayo ya maadili kwa watumishi wa umma yanatolewa na Katibu Msaidizi - Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Ndg.Gerald A.Mwaitebele.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn