DC MAYEKA AWATAKA WADAU KUTUMIA TAFITI KUDHIBITI SUMUKUVU KWA WAKULIMA
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Mayeka Simon Mayeka ametoa wito kwa wadau kutumia matokeo ya tafiti kutoa elimu kuhusu sumukuvu kwa wakulima, walaji na wadau wengine katika sekta ya chakula na lishe.
Mhe.Mayeka amesema hayo leo Mei 20, 2024 Ukumbi wa Veta Kongwa, wakati wa hafla ya mrejesho wa matokeo ya utafiti na mafunzo ya kupunguza sumukuvu katika mazao iliyoandaliwa kwa uratibu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi ya Nelson Mandela.
"Nawapongeza watafiti wote walioshiriki kufanikisha utafiti uliowezesha kupatikana matokeo yatakayo wasilishwa na kujadiliwa wakati wa mafunzo, ambapo zaidi ya kaya 2,874 sawa na idadi ya watu 14,370 wamefikiwa kupitia vituo 52 vya kutolea huduma ya afya ndani ya wilaya yetu ya Kongwa" alisema Mayeka
Aidha, Mayeka ameiomba wizara ya Kilimo kuandaaa mkakati wa makusudi wa kuhakikisha kuwa mapendekezo yote yaliyotokana na tafiti yanafanyiwa kazi kwa ukamilifu.
Naye Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi ya Nelson Mandela Prof.Maulilio Kipanyula ameeleza kuwa, matokeo ya utafiti yaliofanywa na mradi wa MMT yanaendana na yale ya tafiti nyingine zilizofanywa na wanazuoni wengine ambazo pia zilibaini
uwepo wa tatizo la sumukuvu kwenye mazao katika maeneo ya
Wilaya ya Kongwa, na hivyo kuathiri ubora wake kwa matumizi ya
chakula cha binadamu na mifugo.
Mradi wa utafiti wa sumukuvu unaojulikana kama Mycotoxin Mitigation Trial (MMT) umetekelezwa na
Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa na Chuo Kikuu cha Cornell Marekani, kwa ufadhili wa Taasisi ya Bill and Melinda Gates Foundation, lengo kuu ikiwa ni kuchangia katika jitihada za kudhibiti sumukuvu, kwa kufanya utafiti wa
ubora, usalama wa chakula na ukuaji wa watoto wadogo.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

