
MAJALIWA: HONGERENI ASAS KWA USINDIKAJI MAZIWA NCHINI
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa ameridhishwa na maonesho yaliyoandaliwa na Wizara ya Mifugo na uvuvi kwenye viwanja vya Bunge huku akiipongeza kampuni ya kusindika maziwa nchini ya ASAS kwa huduma wanayoitoa kwa jamii.
Majaliwa ameyasema hayo alipotembelea mabanda hayo yaliyopo katika viwanja vya Bunge na kuwataka ASAS waendelee kuhudumia jamii kwa kuzalisha maziwa mengi na Bora.
Waziri Huyo amemuagiza Waziri wa Mifugo na uvuvi Mhe. Abdallah Ulega kuzisaidia kampuni kama ASAS na nyinginezo kwani zinafanya kazi kubwa ya kuzalisha bidhaa ambazo zinaweza kuuzika hata nje ya Nchi.
"Wizara imeonyesha mikakati wa namna inavyoboresha sekta za Mifugo na uvuvi na imethibitisha kiasi cha kuifanya Serikali kuridhia kutenga fedha ya kutosha kwa sekta hizo Mbili na tumeweza kupata mafanikio na tumeona changamoto zilizojitokeza huko nyuma" Alisema Majaliwa.
Aidha,Majaliwa amesema kuwa bado kuna fursa ya wabunge kuchangia maoni kwa sekta hizo mbili na kutoa muelekeo wa kinachopaswa kufanywa na Wizara.
Kwa upande wake Waziri wa Mifugo na uvuvi Mhe. Abdallah Ulega amesema kuwa watahakikisha wanashirikia na ASAS kuhakikisha wanapata maziwa ya kutosha ili kupunguza uaguzaji wa maziwa ya unga.
"Watanzania tumepiga hatua kwani Mifugo na uvuvi ni utajiri unaweza kuinua Pato la Nchi na uchumi wa mtu mmoja mmoja" Alisema Ulega.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa ASAS Fuad Asas amesema Wizara ya Mifugo na uvuvi imewapa ushirikiano hasa katika kusaidia uzalishaji wa maziwa na upatikanaji wa ng'ombe Bora kwa kuwaunganisha na wafugaji wa ng'ombe Bora.
Fuad alisema kuwa ipo haja ya Wizara ya Mifugo kuhakikisha inatoa elimu ya kutosha kwa wafugaji ili kuepusha matatizo yatokanayo na maziwa kutoka kwa ng'ombe kwenda Kwa mlaji.
Kwa upande wake mmoja wa mabalozi wa ASAS Lucas mhuvile maarufu kama Joti amesema kuwa lengo kuu ni kuhakikisha jamii kwa ujumla inapata elimu ikiwa sambamba na kutumia maziwa kwa wingi ili kuimarisha na kuboresha afya zao.
#JordanMediaupdates
Tranding News

Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news