BALOZI YAKUB KUITANGAZA BENJAMIN MKAPA HOSPITAL NCHINI COMORO
Balozi anayeenda kuiwakilisha Tanzania katika visiwa vya Comoro, Said Othman Yakub, amesema ataitangaza Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) nchini Comoro.
Akiongea na uongozi wa BMH leo, Balozi Yakub, amesema wananchi wa Comoro sasa wanaweza kuja Tanzania kupata huduma za afya za kibingwa.
"Wananchi wa Comoro kwa sasa wanafata huduma za afya za kibingwa Ulaya, sasa wananchi wanaweza kuja BMH kupata huduma hizo," amesema Balozi alipokuja kumuaga Mkurugenzi Mtendaji wa BMH.
Balozi Yakub amepata fursa ya kumtembelea mtoto wa kumi (10) kupandikizwa uloto katika Kitengo cha Upandikizaji Uloto cha BMH.
Balozi amesema huduma za kibingwa ambazo ataenda kuzitangaza zaidi ni Upandikizaji Uloto kwa watoto wenye siko seli, Upandikizaji wa Figo kwa watu wenye matatizo ya figo na Matibabu ya Watoto.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa BMH, Dkt.Alphonce Chandika, amemshukuru Mhe Balozi kwa kuitembelea BMH na kujionea huduma.
"Nakushuru Mhe.Balozi kwa kuja kututembelea na kuona huduma hapa Hospitalini," alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

