RAIS SAMIA ATOA MSAMAHA KWA WAFUNGWA 1,082
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan ametoa msamaha kwa wafungwa elfu moja na themanini na mbili(1,082) ambapo wafungwa ishirini na tisa(29) kati yao wameachiliwa huru leo tarehe 26 Aprili 2024, wafungwa ishirini (20) waliohukumiwa adhabu ya kifo wamebadilishiwa adhabu ya kifo kuwa kifungo cha maisha, wafungwa ishirini na saba (27) waliohukumiwa kifungo cha maisha wamebadilishiwa adhabu kuwa kifungo cha miaka thelathini (30) na wafungwa elfu moja na sita (1,006) wamepunguziwa adhabu zao na watabaki gerezani na kuendelea kutumikia sehemu ya kifungo kilichobaki.
.
Rais Samia ametoa msamaha huo leo Aprili 26,2024 katika kuadhimisha sherehe za miaka 60 ya Muungano wa Tanzania.
.
Wafungwa walioachiwa huru ni wale wenye sifa stahiki ya kupunguziwa robo ya adhabu zao wanazozitumikia hivi sasa baada ya kutoa punguzo la kawaida la moja ya tatu linalotolewa chini ya kifungo cha 49 (1) cha sheria ya Magereza sura ya 58.
.
Wafungwa wenye magonjwa ya kudumu au sugu ambao wapo kwenye hatua ya mwisho "terminal stage".
.
Wafungwa wazee wenye umri wa miaka sabini (70) au zaidi, wafungwa wa kike walioingia na ujauzito gerezani au wenye watoto wanaonyonya au waisonyonya.
.
Aidha, Serikali imewataka wafungwa walioachiwa huru leo kushirikiana na wananchi wenzao katika ujenzi wa Taifa letu na kujiepusha na kutenda makosa ili wasirejee tena gerezani.
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

