
TISA (9) WASHINDA TUZO YA TAIFA YA MWALIMU NYERERE YA UANDISHI BUNIFU JIJINI DAR ES SALAAM
Washindi wa Kwanza wa Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu 2024 katika nyanja ya Riwaya, Shairi na Hadithi za watoto.
.
Katika kipengele cha Riwaya, mshindi wa kwanza ni Laura Pettie Kissakwa, mshindi wa pili ni Bishop John Hiluka, na mshindi wa tatu Innocent Ndayanse.
.
Kipengele cha Shairi, mshindi wa kwanza Mohammed Omar Juma,mshindi wa pili Rashid Othman Ali na mshindi wa tatu ni Fabian Martin Fungameza.
.
Na kwenye kipengele cha Hadithi za Watoto, mshindi wa kwanza ni Blandina Isabela Lucas,mshindi wa pili ni Dotto Rangimoto na mshindi wa tatu ni Habybat Abdulhaq Habib.
.
Zawadi walizopewa washindi wa kwanza katika kipengele cha Riwaya ni fedha taslimu shilingi Milioni 10( kwa kila mshindi wa tuzo hiyo) pamoja na ngao, na pia vitabu vyao vya uandishi bunifu vitanunuliwa na serikali na kusambazwa katika shule mbalimbali hapa nchini na kwenye maktaba pia.
.
Na washindi wa pili katika kipengele cha Shairi, kila mshindi amepewa zawadi ya fedha taslimu shilingi Milioni 7.
.
Aidha, Washindi wa tatu katika kipengele cha Hadithi za Watoto,kila mshindi amepewa zawadi ya fedha taslimu shilingi Milioni 5.
Washindi hawa wametangazwa Aprili 13, 2024 Jijini Dar es Salaam katika hafla ya utoaji tuzo hizo ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Prof.Abdurazack Gurnah Mshindi wa Tuzo ya Nobel katika Fasihi Mwaka 2021.
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ilianzisha Tuzo hiyo Mwaka 2023 kwa lengo la kukuza Kiswahili, kutunza historia, kuhamasisha uandishi na usomaji vitabu pamoja na kuinua Sekta ya uchapishaji.
Tranding News

Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news