logo

MIAKA 3 YA RAIS SAMIA IMEKUWA NA MANUFAA MAKUBWA KWA WANAWAKE TANZANIA- MBUNGE VITI MAALUM(CCM) MHE.DITOPILE

MBUNGE wa Viti Maalumu (CCM)Mkoa wa Dodoma Mhe.Mariam Ditopile amesema miaka mitatu ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan,imekuwa na manufaa makubwa kwa wanawake wa Tanzania.

Amesema miongoni mwa mambo ya kujivunia katika kipindi hicho ni pamoja na kuimarishwa kwa huduma za kijamii zinazomgusa mwanamke moja kwa moja na kusaidia kutatua changamoto zao.

Mhe.Ditopile ameyasema hayo leo Machi 25,2024 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma.

"Ndani ya Kipindi kifupi cha Rais Samia ametuheshimisha wanawake kwa kuboresha huduma za ustawi wa jamii, kuchochea maendeleo ya Jinsia na uwezeshaji wa wanawake,kuimarisha upatikanaji wa haki na Maendeleo ya Mtoto, pia ameimarisha utekelezaji wa Mpango kazi wa Taifa wa kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto.

"Rais Samia ni Kinara wa utekelezaji wa eneo la Haki na usawa wa kiuchumi kwa Wanawake na ndiyo maana Serikali ya Awamu ya Sita inatekeleza na kushiriki kwa vitendo Programu ya Kitaifa ya utekelezaji wa Ahadi za Nchi kuhusu Kizazi chenye usawa 2021/2022-2025/2026 (Generation Equality Forum Commitments), alisema Ditopile.

Mbunge huyo amesema utawala wa Rais Dkt.Samia umeongeza kazi zenye staha kwa kuendeleza biashara na urasimishaji wa biashara za wanawake,ameboresha upatikanaji na matumizi ya teknolojia nafuu na zinazofaa ili kuongeza Uwezo wa wanawake wa kuzalisha bidhaa zenye Ushindani wa Soko la ndani na nje.

.

Aidha,Kwa mujibu wa Mhe.Ditopile, Rais Samia katika kuhakikisha kuwa haki za wanawake na hasa wajane zinapatikana hapa nchini Kampeni ya huduma ya msaada wa kisheria ya "MAMA SAMIA" ambayo ni mojawapo ya afua za programu ya kizazi chenye usawa yenye lengo la kulinda na kukuza haki ya upatikanaji wa huduma za Msaada wa kisheria Nchini.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn