NELSON MANDELA YAWEKEZA KWENYE HISABATI NA SAYANSI SHULE ZA NGANANA NA NAMBALA ARUSHA
Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela kupitia Kituo cha Ubora cha Tehama Afrika Mashariki, (CENIT@EA) wametoa uenezi na huduma kwa jamii katika shule mbili za msingi Nganana na Nambala zilizopo Halmashauri ya Arumeru jijini Arusha lengo ikiwa ni kuhamasisha umuhimu wa kuweka mkazo katika masomo ya Sayansi na Hisabati.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo katika shule hizo ,Machi 21,2024 Mhadhiri na Mratibu wa Uhusiano ya Kitaaluma na Viwanda na wa Sayansi katika Mifumo iliyopachikwa na Simu (EMoS) Dkt.Judith Leo akiwa ameongozana na wanafunzi wa Shahada ya Umahiri (EMoS) amewaeleza wanafunzi hao kuwa, masomo ya Sayansi na Hisabati sio magumu kama ambavyo wanafikiri ila juhudi binafsi na kupenda somo kunaweza kuwafanya wafaulu vyema.
Aidha,Wanafunzi wa Shahada ya Umahiri katika Mifumo Iliyopachikwa na Simu (EMoS) walitoa elimu kwa vitendo wa namna ya kutumia vifaa mbalimbali vya kisayansi ikiwemo kompyuta, vifaa vya maabara katika kutambua matatizo mbalimbali yanayoikabili jamii ili kuwapata ufumbuzi wa kutatua changamoto hizo.
Naye, Mwanafunzi wa Shahada ya Umahiri katika Mifumo Iliyopachikwa na Simu (EMoS) Seth Odwar kutoka nchini Kenya amewahimiza wanafunzi hao kuzingatia somo la Hisabati ambalo wengi huhisi halina manufaa katika kozi nyingine na kuongeza pia Sayansi ni muhimu katika kutatua changamoto za jamii.
Akizungumza kwa niaba ya Wanafunzi wenzake Jackline Mushi ameishukuru Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela kwa kutoa hamasa kwa vitendo pamoja na kuwajengea uwezo katika matumizi ya vifaa vya kisayansi ikiwemo kompyuta.
Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela inatekeleza majukumu yake katika misingi mitano (5D Business Modal) mojawapo ya msingi huo ni Uenezi na Huduma kwa Jamii (Outreach na Community Engagement).
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

