DKT.BITEKO AZINDUA RAFIKI HOTEL DODOMA, AMSIFU MMILIKI WA HOTELI HIYO BW.MALLYA
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe.Dkt.Doto Biteko amesema Rais Dkt.Samia amejipambanua kama mlezi wa Sekta binafsi nchini na hataki kuona wafanyabiashara wanapata misukosuko wakati wa utekelezaji wa majukumu yao.
Dkt.Biteko amesema hayo jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa Rafiki Hoteli ambao uliohudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda.
Aidha,Dkt.Biteko amewaagiza watendaji wa Serikali kuhakikisha wanailea Sekta binafsi na kila mtu atimize wajibu wake kwenye eneo lake.
“kama wewe ni Afisa wa TANESCO uliye na wajibu wa kumuunganishia mfanyabiashara umeme ambao mwisho wa siku ataulipia kwa ajili ya mapato yako,huna sababu ya kumwambia njoo kesho wakati kazi hiyo ungeifanya leo.”
Amesema Watendaji ambao ni warasimu lazima waone aibu kwa kuchelewesha shughuli zinazoijenga nchi.
Dkt.Biteko amesema kuwa,Rais Dkt.Samia anataka kuona watanzania wakiwa kwenye daraja la kwanza katika nchi yao na pia waweze kufanya uwekezaji ndani na nje ya nchi bila vikwazo vyovyote.
Kuhusu Sekta ya Utalii nchini,amesema bado kuna changamoto ya upungufu wa vitanda kwa wageni wa ndani na nje ya nchi hivyo bado kuna kazi kubwa ya kuwekeza kwenye sekta ya _hospitality_ ambapo amewapongeza wamiliki wa Rafiki hoteli na wawekezaji wengine ambao wanaifanyia kazi changamoto hiyo.
Vilevile,Biteko ameipongeza menejimenti ya hoteli hiyo kwa kutekeleza dhana ya nishati safi ya kupikia kutokana na kuweka miundombinu ya nishati safi ya kupikia kwenye hoteli hiyo na kutoa wito kwa wananchi kutoharibu mazingira na kutokukata miti kwa ajili ya matumizi ya kuni na mkaa.
.
Kutokana na hilo ameagiza Watendaji wa Serikali kuhakikisha kwamba shughuli zinazoweza kufanyika ndani ya Mkoa wa Dodoma zifanyike katika Mkoa husika ili pia kutoa fursa kwa wananchi kupata huduma muda wote pale wanapohitaji huduma za watendaji hao.
Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu na Mmiliki wa Rafiki Hoteli Fladmiry Mallya ameishukuru Serikali kwa kuweka mazingira bora ya uwekezaji ambayo yanafanya Watanzania kuendelea kuwekeza kwenye nchi yao na hivyo kuwa na mchango katika ukuaji wa uchumi wa nchi na kukuza ajira.
@rafikidodomahotel
#JordanMediaUpdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news