logo

PROF.NDALICHAKO AKABIDHI MASHAMBA NA VITENDEA KAZI KWA VIJANA 268 WA BBT

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof.Joyce Ndalichako (Mb) amekabidhi mashamba na vitendea kazi kwa vijana 268 waliopo kwenye programu ya Building a Better Tomorrow (BBT) katika eneo la Chinangali- Dodoma, tarehe 22 Januari 2024.

.

Prof.Ndalichako Amesema Leo ni siku ambayo maono ya Mhe. Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan yanaenda kutimia kwa kuwa vijana 268 wanaanza kazi rasmi ya kuisaidia Tanzania kuilisha Dunia, hivyo watambue kuwa wanaenda kuzalisha chakula kwa manufaa ya nchi na ya kwao binafsi.

.

Kwa upande wake Waziri wa Kilimo Mhe.Hussein Bashe amesema;

"Niliamua kusikiliza maoni kinzani, ili kuhakikisha maoni hayo yanatumika kuendeleza BBT hii ambayo leo vijana wanakabidhiwa rasmi mashamba ya Chinangali,”.

.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo, Mhe. Deo Mwanyika (Mb) amewataka vijana hao kuhakikisha wanafanya kazi na kutimiza malengo ya programu hiyo kwa kuwa fedha zilizowekezwa hapo ni za Umma na zinatakiwa kuonesha mafanikio.

"BBT ikifanikiwa ni kuwa wanafanikiwa Watanzania, sasa lazima muweze kufanikisha malengo ya programu hii,” Alisema.

.

Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali ikiwemo Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara,Mhe.David Silinde (Mb), Naibu Waziri wa Kilimo; Bw.Gerald Mweli, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Wakuu wa Taasisi za Wizara na Wadau kutoka Benki za TADB na NMB.

@wizara_ya_kilimo

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn