MCHUNGAJI NCHINI ZAMBIA AMPIKA MUUMINI WAKE ILI ASICHEPUKE NJE YA NDOA
Mchungaji mmoja nchini Zambia(jina halijafahamika) amefanya maamuzi ya kumpika mmoja wa washirika wake wa kiume katika moto wakati wa ibada kanisani.
Kulingana na habari za moja kwa moja, mshirika huyo alitoka nje ya ndoa na ndipo mkewe huyo alipoamua kumripoti kwa mchungaji huyo.
Baada ya kuandaa kikao cha ushauri nasaha kwa ajili yake na mkewe, mchungaji huyo aliamua kulipeleka suala hilo kwenye ulimwengu wa kiroho.
.
Na kwa mujibu wake, Mungu alimwambia ampike kwenye sufuria mume huyo asiye mwaminifu ili aache kutoka nje ya ndoa.
Katika picha mume huyo asiye mwaminifu alionekana akiwa amekaa kwenye sufuria kubwa na mchungaji akiwa amesimama karibu yake.
Mmoja wa waumini wa kanisa hilo alikuwa akimmiminia kitunguu, pilipili na nyanya kwenye sufuria katika maandalizi ya kumpika.
Jamaa huyo ambaye aliona aibu aliinamisha kichwa chini akiwa amekaa kwenye sufuria huku waumini wengine wakimtazama.
.
Upi Mtazamo wako mtu wangu...!! Ebu tuambie hapo chini kwenye Comments 😁😁.
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news