logo

BASHE AZINDUA BODI CHUO CHA TAIFA CHA SUKARI

WAZIRI wa Kilimo, Mhe.Hussein Bashe leo April 25, jijini Dodoma amezindua Bodi ya Chuo cha Taifa cha Sukari na Kukitaka Bodi hiyo kuhakikisha kuwa inakuwa Kituo cha Umahiri cha kutumika kuboresha sekta ya sukari nchini.

Katika uzinduzi huo uliofanyika kwenye Ukumbi wa Wizara ya Kilimo-Dodoma na kuhudhuriwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Bw. Gerald Mweli,Waziri Bashe ameitaka Bodi hiyo kuhakikisha inatanua zaidi utendaji kazi wa chuo kutoka kuwa cha kuwafundisha wanafunzi na kuwa nguzo muhimu ya mabadiliko ya sekta ya sukari.

"Chuo hiki kinatakiwa kuwa Kituo cha Umahiri ambapo kiwe ndio mahala pa kuchangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya kilimo cha sukari, nataka kiwe kina uwezo wa kusaidia katika kuongeza thamani ya sukari, kisaidie mbinu za kibunifu kwa kampuni za sukari ili zizalishe sukari za matumizi ya kawaida na za viwandani yani chuo isiwe tu ni kuhusu wanafunzi peke yake" amesema Bashe.

Ameiagiza bodi hiyo kuhakikisha kuwa chuo kinafanya kazi kwa ukaribu na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania(TARI) na wadau wengine katika kilimo kuhakikisha wakulima wadogo na wakubwa wa miwa wanalima kwa tija.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn